Wakati viongozi hususani wa kuteuliwa wakitakiwa kuzingatia ukweli kwamba serikali ya awamu hii haihitaji wanaoficha mabaya wakitaka mazuri ndiyo yaonekane, baadhi wameshauri mfumo uliopo, hususani wa kupeana taarifa uangaliwe kwa kuwa una tatizo linalohitaji kufanyiwa kazi.
Miongoni mwa watu ambao walizungumza jana kuhusu hatua hiyo ya Rais kutengua uteuzi wa Kilango, ni mwanasiasa mkongwe nchini, Paul Kimiti aliyetaka viongozi wengine kutambua kwamba, Magufuli ni kiongozi asiyependa unafiki.
“Uongozi wake tangu mwanzo umejidhihirisha wazi kuwa ni kiongozi anayependa uwazi na ukweli hataki short cut (njia za mkato),” alisema Kimiti.
Kimiti aliyewahi kushika uwaziri katika Serikali zilizopita, alisema hatua hiyo ya Rais ni ishara na funzo kwa viongozi wengine hasa wale walio madarakani kuhakikisha kuwa wanawajibika ipasavyo kwa kufuata misingi ya uwazi na kutokimbilia njia za mkato.
Kwa upande wa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, alisema hatua aliyoichukua Dk Magufuli ya kumvua uongozi Kilango ni ishara kuwa anatoa kipaumbele katika suala zima la uwajibikaji lakini pia hapendi viongozi wasiojishughulisha.
“Inaonesha dhahiri Dk Magufuli katika masuala nyeti yanayogusa taifa hapendi majibu mepesi wala njia za mkato. Hii inamaanisha kuwa viongozi hawana budi kuzifanyia kazi taarifa wanazopewa na kujiridhisha kwanza,” alisema Dk Bana.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment