Mkuu
wa wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewasimamisha kazi maofisa watano
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za
umma na matumizi mabaya ya madaraka.
Akiwa
katika ziara ya siku moja ya kujitambulisha wilayani Ilemela leo,
Mongella ameagiza kushushwa cheo kwa ofisa wa ardhi wa wilaya hiyo,
Anicet Rweyemamu kwa tuhuma za kushindwa kusimamia watumishi walio chini
yake wanaotuhumiwa kupokea Sh12 milioni kutoka kwa mwananchi mmoja
aliyekuwa akitaka ardhi, lakini hajapewa hati hadi sasa.
Wengine
walioangukiwa na rungu la mkuu huyo ni Debora Tongora ambaye pamoja na
Alex Chigulu wanatuhumiwa kupokea fedha hizo kutoka kwa wananchi kwa
ahadi ya kuwapatia viwanja.
Wakati
Tongola tayari amefunguliwa mashtaka dhidi ya tuhuma hizo, Chigulu
amehamishiwa mkoani Singida lakini Mongella ameagiza arejeshwe Mwanza
ili afikishwe mahakamani.
“RPC
wasiliana na mwenzako wa Singida ili huyo mtumishi atiwe mbaroni muda
huu na kesho arejeshwe Mwanza kukabiliana na mashtaka dhidi yake.
Hatuwezi kuwavumilia watumishi wanaoharibu sehemu moja halafu wanakimbia
uhamisho kwenye maeneo mengine,” amesema Mongella
Ofisa uvuvi wa Kituo cha Kirumba, Ivon Maha ameshushwa cheo huku Peter Revelian akiondolewa kutoka nafasi ya mweka hazina.
Watumishi
hao wa Idara ya Uvuvi wameondolewa madarakani baada ya kutuhumiwa
kuhusika na upotevu wa zaidi Sh40 milioni zilizotokana na kodi na
ushuru.
Awali,
Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Manju Msambya alimweleza Mongella kuwa
wilaya hiyo tayari imetengeza madawati 7, 200 kati ya 29, 000
yanayohitajika.
“Wilaya yetu inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu katika shule za umma na tayari tumewasilisha maombi ya walimu wapya,” amesema Msambya
Meya
wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulungi alimuahidi mkuu huyo wa mkoa
kuwa baraza lake litaongeza juhudi katika usimamizi wa utendaji kwa
watumishi wa halmashauri hiyo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment