Hayo
yalisemwa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, kupitia
taarifa aliyoitoa kwa Bunge baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo
Peneza (Chadema) kumuomba Rais John Magufuli kujipunguzia mshahara.
Mbunge
huyo aliyasema hayo wakati akijadili Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa
2016/17 hadi 2021, ambapo pamoja na kusifu jitihada za Rais Magufuli kwa
kuonesha dhamira ya wazi ya kuwajali wananchi masikini na kudhibiti
matumizi ya serikali, alimuomba kupunguza mshahara wake na pia kuruhusu
ukatwe kodi.
“Kwa
kweli kwa dhati kabisa nampongeza sana Rais Magufuli kwa namna
anavyoonesha wazi kwamba ana dhamira ya kuwatumikia Watanzania. Kwa
namna anavyokwenda ni wazi kwamba Rais Magufuli anakuwa Rais wa pili
kuwa na mapenzi ya dhati kwa Watanzania baada ya Rais Nyerere (Julius-
Baba wa Taifa).
“Pamoja
na hayo, kama anataka awe kama Mwalimu Nyerere basi ni wakati sasa wa
Rais Magufuli kuchukua hatua za kujipunguzia mshahara wake na pia
kuruhusu mshahara wake kukatwa kodi, hili litampa heshima kubwa sana
Rais wetu,” alisema Peneza.
Akitoa
taarifa kwa Bunge, Waziri Simbachawene alisema kwa mujibu wa Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 pamoja na marekebisho
yake, Ibara ya 43, Ibara ndogo ya 3, Ukurasa wa 62 inamzuia Rais
kupunguza mshahara akiwa madarakani.
Alisema; “Ibara hiyo inasema hivi: ‘Mshahara na malipo ya Rais, havitapunguzwa wakati Rais anapokuwa bado anashika madaraka yake.
“Rais
aliyepo sasa hawezi kujipunguzia mshahara wake yeye mwenyewe isipokuwa
anapoondoka anaweza kuweka kiwango cha mshahara cha Rais ajaye.
"Kwa hiyo wakati wabunge mnaendelea kumuomba Rais apunguze mshahara wake ni lazima mjue jambo hilo ni kinyume cha Katiba”.
Ufafanuzi
huo wa Waziri umekuja siku chache wakati Rais Magufuli akiwa tayari
amejitangazia mbele ya umma kiwango cha mshahara anacholipwa akisema ni
Sh milioni 9.5 kwa mwezi.
Rais
aliyasema hayo akiwa nyumbani kwake Chato mkoani Geita wakati
alipokwenda kwa mapumziko mafupi hivi karibuni, hatua ambayo ilipokelewa
kwa shangwe na wananchi wengi
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment