Gari lenye mwili wa marehemu ,Amatus Liyumba ukiwasili leo mchana Nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likishushwa kwenye gari tayari kwa ajili ya kuingizwa nyumbani kwake.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo ( watatu
kushoto) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa Marehemu, Amatus
Joachim Liyumba nyumbani kwake mikocheni.
Padri wa Kanisa la Mtakatifu Michael, Kawe jijini Dar, Fr. Nicholas Kundyaj akiendesha ibada fupi msibani hapo.
HATIMAYE mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi
na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania ( Bot), Amatus Liyumba, leo umeagwa
katika nyumba yake iliyopo Mikocheni B, jijini Dar.
Akizungumza na GPL, mpwa wa marehemu, Arbogasti Chiwembo, alisema marehemu mjomba wake alifariki Aprili 18,
mwaka huu katika Hospitali ya Agha Khan kutokana na maradhi ya
kisukari na shinikizo la damu. Ameacha watoto saba na mwili wake
utasafirishwa kesho alfajiri kuelekea Mahenge mkoani Morogogo kwa ajili
ya mazishi.
Marehemu Liyumba aliwahi kukabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya
ofisi kati ya mwaka 2001 na 2006 wakati wa ujenzi wa majengo pacha ya
makao makuu ya BoT, ambapo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu kwa kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 221.
Habari :Gabriel Ng`osha na Denis Mtima/GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]








0 comments:
Post a Comment