RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara 13 za
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mawaziri wasiokuwa na Wizara
Maalum ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.
Hafla
hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa
na viongozi mbali mbali wa vyama na Serikali pamoja na wananchi kadhaa
ambapo miongoni mwa waliohudhuria ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif
Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza
la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid.
Wengine
ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, Kadhi Mkuu wa
Zanzibar Sheikh Khamis Haji na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.
Abdalla Mwinyi Khamis. Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib
Abrahman Khatib pamoja na viongozi wa vikosi vya Ulinzi.
Walioapishwa
katika hafla hiyo ni Waziri, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi Gavu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali
Suleiman. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum
za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed, Waziri wa Afya
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.
Riziki Pembe Juma pamoja na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico.
Wengine
ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali,
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Balozi Ali Abeid A.
Karume. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid
Mohammed. Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali
Juma na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Salama Aboud
Talib.
Kwa
upande wa Manaibu Waziri ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Katiba,
Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Khamis Juma Maalim. Naibu
Waziri wa Afya Mhe. Harusi Said Suleiman na Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali, Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.
Wengine
ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Mohammed
Ahmed Salum. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo nan Uvuvi Mhe.
Lulu Msham Abdulla, Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo
Mhe. Bibi Choum Kombo Khamis na Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na
Mazingira Mhe. Juma Makungu Juma.
Aidha,
Dk. Shein amewaapisha Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri
Wasiokuwa na Wizara Maalum akiwemo Mhe. Said Soud Said kuwa Mjumbe wa
Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum pamoja na Mhe.
Juma Ali Khatib Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na
Wizara Maalum.
Kwa
uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42, 43,44 na 47 vya Katiba ya Zanzibar
ya mwaka 1984, Dk. Shein ameunda Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na kuwateua Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara hizo pamoja
na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum na Wajumbe wa Baraza la
Mapinduzi.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment