Mahakama
ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imemhukumu kwenda jela miaka 12,
Qasama Machibya aliyejifanya ofisa usalama wa Taifa kwenye ziara ya Rais
wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete mwaka 2013.
Kabla
ya hukumu, mshtakiwa alijitetea mahakamani hapo kuwa kitambulisho
alichokutwa nacho siyo chake na anashangaa kuona kuna picha yake na jina
lake.
Alidai kuwa hizo ni mbinu za polisi kumminya, hivyo aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu na kwamba ana ugonjwa wa Ukimwi.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Kurwijila alisema utetezi wa
mshtakiwa hauifanyi mahakama kutomtia hatiani kwa kuwa hana cheti cha
ugonjwa.
Alisema kutokana na mahakama kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka uliowasilishwa inamtia hatiani kwa makosa matatu.
Kurwijila
alisema kosa la kwanza ni kughushi nyaraka ya Serikali hivyo, atakwenda
jela miaka mitano na kosa la pili la kujifanya ofisa usalama wa Taifa
kifungo chake ni miaka miwili.
Alisema katika kosa la tatu la kuudanganya umma kwa kutoa nyaraka iliyoghushiwa hivyo, atatumikia adhabu gerezani miaka mitano.
Mwendesha
Mashtaka wa Polisi, Elias Mgobela alisema mshtakiwa alikamatwa wakati
Kikwete alipokuwa akitarajia kuhutubia wananchi kwenye mkutano wa
hadhara.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment