Mahakama
ya Rufani jana ilianza kusikiliza rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa
Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP) Abdallah Zombe na askari wenzake wanane kuhusu kesi ya mauaji
waliyoshinda.
Katika
kesi hiyo namba 358 ya mwaka 2013, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)
anapinga Zombe na wenzake kuachiwa huru na Mahakama Kuu katika kesi ya
mauaji ya watu wanne iliyokuwa ikiwakabili.
Zombe
na maofisa wenzake walifunguliwa mashtaka katika Mahakama Kuu wakidaiwa
kuwaua watu wanne wakiwamo wafanyabiashara watatu wa madini kutoka
Mahenge, Morogoro, Januari 14, 2006.
Mauaji
hayo yalifanyika katika msitu wa Mabwepande, Dar es Salaam na waliouawa
walikuwa Mathias Lunkombe, Sabinus Chigumbi maarufu kwa jina la Jongo
pamoja na ndugu yake Ephrahim Chigumbi na dereva teksi, Juma Ndugu wa
Manzese.
Mahakama Kuu katika hukumu yake ya Agosti 17, 2009 iliwaachia huru washtakiwa wote baada ya kuwaona hawana hatia.
Mahakama Kuu katika hukumu yake ya Agosti 17, 2009 iliwaachia huru washtakiwa wote baada ya kuwaona hawana hatia.
DPP
hakuridhika na hukumu hiyo na mwaka huohuo, alikata rufaa Mahakama ya
Rufani akidai jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo alikosea kuwaachia
huru washtakiwa hao, na kwamba kulikuwa na ushahidi wa dhahiri na wa
kimazingira wa kutosha kuwatia hatiani washtakiwa wote.
Rufaa hiyo pia ilitupiliwa ambali na Mahakama Mei 8, 2013 kutokana na dosari za kisheria zilizobainika kwenye rufaa hiyo.
Baadaye DPP alipeleka maombi Mahakama Kuu aruhusiwe kukata tena rufaa hiyo nje ya muda, ombi ambalo lilikubaliwa.
Hata
hivyo, katika shauri hili jipya DPP amewaondoa wajibu rufani watano
baada ya kubaini kuwa ushahidi alionao hauwagusi katika rufaa hiyo.
Waliosalia pamoja na Zombe ni Christopher Bageni, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari lakini walioondolewa ni Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Abineth Salo na Festus Gwabisabi.
Waliosalia pamoja na Zombe ni Christopher Bageni, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari lakini walioondolewa ni Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Abineth Salo na Festus Gwabisabi.
Katika
rufaa hiyo iliyosikilizwa jana na majaji Bernard Luanda, Sauda Mjasiri
na Semistocles Kaijage, DPP anapinga hukumu iliyowaachia huru.
Wakati
wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, Wakili wa Serikali, Timon Vitalis
aliieleza Mahakama kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani wajibu
rufani hao kwani unadhihirisha walikuwa na nia moja ya kutenda kosa
pamoja na mtenda kosa halisi (Koplo Saad Alawi aliyetoroka).
Alisema
kuwa kitendo cha wajibu rufani hao ambao ni maofisa wa polisi wenye
wajibu na uwezo wa kuzuia uhalifu kuwapo eneo la tukio la mauaji
wakashuhudia na kushindwa kuzuia ni dhahiri kuwa walikuwa na nia moja na
mtenda kosa.
Kuhusu
Zombe, Vitalis alisema kitendo cha kuwaelekeza watuhumiwa namna ya
kueleza (walipoitwa kuhojiwa kwenye Tume ya Rais) na kutangaza kuwa watu
waliouawa waliuawa kwenye mapambano na polisi ni dhahiri alikuwa
akimsaidia mtenda kosa kusema uongo ili kumlinda.
Wakijibu
hoja hizo kwa nyakati tofauti, mawakili wa utetezi walisema hakuna
ushahidi wa dhahiri wa kuwatia hatiani wajibu rufani hao na kwamba
Mahakama Kuu ilitathmini vema na kujiridhisha kuwa hawana hatia.
Hivyo
waliiomba Mahakama hiyo iwaone kuwa hawana hatia kwa mashtaka
yanayowakabili, huku Wakili Dennis Msafiri akisisitiza kuwa Jamhuri
inapaswa kutumia nguvu nyingi kumtafuta muuaji halisi kama
walivyoelekezwa na Mahakama Kuu na si kutumia muda mwingi kuendelea
kuwang’ang’ania wajibu rufaa.
Baada
ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Luanda aliahirisha shauri hilo
akisema kuwa wanakwenda kutafakari hoja za pande zote na kwamba
wanahitaji muda kuandika uamuzi ambao watautoa pale utakapokuwa tayari.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment