Maryland, Marekani
WANASAYANSI kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Moyo, Mapafu na Damu huko Maryland nchini Marekani wanasema kuwa wamefanikiwa kuweka moyo wa nguruwe katika nyani kwa zaidi ya miaka miwili.
Matokeo yake yanaweza kupiga hatua
katika tiba ya upandikizaji wa viungo vya wanyama katika binaadamu huku
kukiwa kuna upungufu wa binadamu wanaotoa viungo vyao.
Upandikazi wa viumbe tofauti husababisha
mmenyuko wa kinga na kusababisha kukataliwa kwa kiungo hicho na mwili
unaofanyiwa upasuaji huo.
Lakini wanasayansi kutoka Marekani na
Ujerumani walitumia muundo wa jeni pamoja na dawa zinazopunguza kinga.
Kazi yao imeelezea katika jarida la mawasiliano ya kiasilia.
Ni muhimu kwa sababu inaleta uwezekano
wa kutumia viungo hivyo kwa binaadamu, kulingana na mwandishi mwenza
Muhammad Mohiuddin kutoka Maryland, alikiambia chombo cha habari cha
AFP.
Upandikizaji wa kutumia viumbe tofauti
unaweza kuokoa maisha ya wengi kila mwaka ambayo hupotezwa kutokana na
ukosefu wa viungo vya binaadamu kwa upandikizaji.
CHANZO NA BBC SWAHILI
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment