Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wajumbe
wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuzingatia mahitaji mapya na changamoto
zilizojitokeza baada ya kuunda Kamati hizo mwezi Januari 2016.
Mabadiliko
hayo, yamefanywa chini ya Kanuni ya 116(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge
inayompa Mamlaka ya kuteua Wabunge kuunda Kamati Mbalimbali za Bunge.
Aidha
kufuatia mabadiliko hayo ambayo baadhi yake yamehusu Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti au wote wawili, Kamati za Kudumu za Bunge zilizoathirika na
mabadiliko haya zitawajibika kufanya Uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa
kanuni ya 116 (10) kama ifuatavyo:
- Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii itahitaji kupata Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wapya.
- Kamati ya Nishati na Madini itahitaji kupata Mwenyekiti mpya.
- Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma itahitaji kupata Mwenyekiti mpya.
- Kamati ya LAAC itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya.
- Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya.
Mabadiliko haya kwenye kamati zote yanaanza mara moja ambapo orodha ya wajumbe waliobadilishwa imeambatishwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment