Mojawapo ya magari yaliyohusishwa katika ajali iliyotokea leo asubuhi eneo la Bamaga, Dar likiondolewa eneo la ajali.
Magari yaliyohusishwa kwenye ajali hiyo yakiwa eneo la tukio.
Taswira kutoka eneo hilo.
Polisi wa usalama barabarani wakichukua baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo.
MAGARI mawili yenye namba za usajili T 300
ASH na T 173 CJD yote aina ya Toyota Carina leo asubuhi yamegongana eneo
la Bamaga jijini Dar es Salaam na kujeruhi watu waliokuwemo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 asubuhi ikiyahusisha magari hayo.
“Mimi nilikuwa jirani na Bamaga, lakini
ghafla nilisikia kishindo kikubwa kikitokea eneo la ajali, nilipokimbia
kwenda kuangalia kuna nini nikakuta ajali ya magari haya mawili madogo
ambayo yamegongana na watu waliokuwemo ndani wakilalamika kwa maumivu.”
Alisema shuhuda huyo aliyejitambulisha kwa jina la Edward.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa kwenye Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kwa matibabu.
Picha na Shabani Chuck / GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment