Mahakama
ya Hakimu mkazi Arusha imempa dhamana Mtuhumiwa Isaac Abakuki
anayetuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kupitia kwenye ukurasa wake
kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Hakimu
mfawidhi Agustino Rwezire amesema Mahakama baada ya kupitia hoja mbili
zilizotolewa na upande wa mashtaka na mshtakiwa, imeridhia kutoa
dhamana kama haki ya msingi ya mshtakiwa kutokana na kosa alilotenda
ambapo dhamana hiyo ni ya Wadhamini wawili waliotakiwa kuwa na jumla ya
shilingi milioni tano.
Kwenye
siku ya kwanza kufikishwa Mahakamani Polisi walisema Tarehe 17 March
2016 Isaac Abakuki akiwa nyumbani kwake Olasiti Arusha alipokea ujumbe
kwenye account yake ya Facebook ukisema ‘mnamlinganishaje Magufuli na
Nyerere’ ukiwa ni Ujumbe wa mjadala ulioanzishwa kwenye mtandao wa
kijamii kufuatia hatua ya Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha
Clouds 360 CloudsTV na kuwapongeza Watangazaji wa kipindi hicho.
Baada ya kusoma huo ujumbe Mtuhumiwa aliandika comment kujibu alichokisoma na kuandika ; ‘Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi buana“….. comment
ya mtuhumiwa iliwaudhi na kuwakwaza watu wengi walioona Facebook na
wakaamua kufikisha malalamiko yao kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania
TCRA.
TCRA
kwa kushirikiana na Polisi baada ya kufanya uchunguzi wa kina
walifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa 22 March 2016 kwenye hoteli ya Annex
Arusha na alipandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza April 15 2016, kesi
yake itaendelea tena May 17 2016.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment