Chama Cha Abiria Nchini Chawataka Wamiliki wa Mabasi Kuwahudumia Majeruhi Pindi Inapotokea Ajali

Chama cha kutetea haki za abiria nchini(CHAKUA),imeitaka serikali kuwabana wamiliki wa magari ya abiria,pindi magari yanapopata ajali na kusababisha majeruhi wa abiria,ili kuwagharimia matatibu na fidia.

Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Hassan Mchanjama amesema kuwa, kutokuwa na usimamiaji wa kuridhisha kwa vyombo hivyo,imekuwa ukisababisha umekosaji wa haki za abiria pindi wanapopata ajali.

Bwana Mchajama amesema kuwa hali imekuwa ikisababisa malamiko mengi kutoka kwa wahanga wa ajali wa mabasi,na hata pindi wakati wakitaka kupewa haki zao wamekuwa wakizikosa.

Kwa upande mwingine amesema kuwa CHAKUA wamebaini kuwa kuwa watu wengi wanaopata ajali hukosa haki zao kufuatilia kutozijua sheria za usafiri.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment