CONFIRMED: Yaya Toure Bye Bye Manchester City… Kesho Kutwa Tu Anaondoka

Ni kitambo toka tuanze kusoma vichwa vya habari kwenye Magazeti vikisema ….Yaya Toure kuondoka Man City >>> <<< Man City wamuahidi Yaya Toure asiondoke <<< 
Baada ya hivyo vichwa vya habari, taarifa iliyothibitishwa April 4 2016 na wakala wa Yaya inasema hivi >>> ‘Tumesubiri kwa muda mrefu lakini Man City hawajatekeleza chochote kwenye ahadi walizotoa kwahiyo Yaya ataachana na hii club June 

Yaya amekasirishwa lakini yeye ni mchezaji Professional hivyo ataendelea kushiriki kwa ubora wake chini ya mkataba wa Manchester City mpaka akiondoka‘ – Wakala Dimitri Seluk
Option kubwa aliyonayo Yaya Toure aliyejiunga na City mwaka 2010 akitokea FC Barcelona inatajwa kuwa Inter Milan ambayo iko chini ya kocha Roberto Mancini japokuwa mchezaji huyu amekua na ofa nyingi kwenye meza na inabaki yeye tu kuchagua.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment