Chama
cha Wananchi (CUF) kimemuomba, Rais John Magufuli na Waziri Mkuu, Kasim
Majaliwa, kutumia busara kumaliza mgogo wa umeya katika jiji la Tanga
kama ilikuwa kwenye mgogoro wa umeya jiji la Dar es Salaam na kuagiza
uchaguzi huo urudiwe.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa
CUF Tanzania Bara, Magdalena Sakaya, alisema chama hicho hakimtambui
meya aliyeko hivi sasa kwa madi kuwa si mshindi halali katika uchaguzi
uliofanyika Desemba 19, mwaka jana.
Alidai
katika uchaguzi huo, mgombea wa CUF, Rashid Jumbe, ndiye aliyeshinda
dhidi ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Seleman Mustafa, lakini
ushindi wake uliporwa na msimamizi wa uchaguzi huo kwa kutangaza matokeo
tofauti.
Sakaya alisema kilichotokea katika uchaguzi huo ni uporaji wa matokeo, jambo ambalo limesababisha meya huyo kutokubalika.
“Kutokana
na mvurugano uliopo katika suala hilo, shughuli za maendeleo katika
jijini la Tanga zimesimama na tangu kufanyika kwa uchaguzi huo hakuna
kikao hata kimoja cha baraza la madiwani kilichofanyika kwa sababu
madiwani wa CUF wamegoma kushiriki,” alisema.
“CUF
inamuomba Rais Magufuli ama Waziri Mkuu kutumia busara kama zile
zilizotumika kumaliza mgogoro wa umeya Dar es Salaam ili vikao vya
baraza la madiwani viweze kuanza na kuharakisha shughuli za maendeleo ya
jiji,” alisema Sakaya.
Kwa
upande wake, Mbunge wa Tanga Mjini (CUF), Mussa Mbarowe, alisema ana
amini Rais atatumia busara kumaliza mgogoro huo ili kuwanusuru wananchi
wa jiji hilo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment