DK SHEIN- HATUNA TAARIFA YA KUFUTIWA MISAADA NA NCHI WAHISANI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), haijapokea taarifa ya kufutiwa misaada kutoka kwa nchi wahisani, mbali na taarifa ya kujitoa kwa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC).
Alisema hayo jana baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri na kusisitiza kuwa, pamoja na kutokuwa na taarifa hiyo, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, zimejiandaa kutumia rasilimali zake za ndani kuleta maendeleo.
Kwa mujibu wa Dk Shein, misaada ni njia moja ya kusaidia kuleta maendeleo lakini si ya lazima.


Alisema, SMZ imejipanga kuhakikisha inatumia vizuri rasilimali zake kwa kukusanya mapato na kufanya kazi kwa ufanisi na ubunifu wa hali ya juu.
“Hatujapata taarifa ya kusitishiwa misaada kutoka kwa wahisani, hata hivyo, tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatumia rasilimali zetu, taasisi zinazokusanya mapato nchini na Bodi ya Mapato zitakusanya mapato kikamilifu, ikiwa ni njia moja ya kupunguza utegemezi,” alisema.


Kauli hiyo ya Dk Shein imekuja siku chache baada ya Jumuiya ya Ulaya (EU), kukanusha habari zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii na kwenye baadhi ya magazeti kuwa wadau wa maendeleo, ikiwemo nchi zilizoko katika jumuiya hiyo, wamejitoa kuchangia bajeti ya Tanzania.

Balozi wa EU, anayeongoza umoja wa nchi 28 ambazo ni miongoni mwa wachangiaji wakubwa wa bajeti ya Serikali, Roeland van de Geer alisema, ingawa hajafurahia kilichotokea Zanzibar, lakini hawajafikia uamuzi wa kusitisha misaada kwa Tanzania.
Balozi huyo alisema, kwa uelewa wake, hata Marekani haijajitoa, ila kilichotokea ni MCC ya nchi hiyo kusitisha uhusiano wake na Tanzania.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment