Simba itacheza na Coastal Union Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mchezo wa robo fainali Kombe la FA na ikishinda itaungana na timu za Mwadui FC, Yanga na Azam ambazo tayari zimetinga nusu fainali.
Mayanja amesema timu zote ambazo zimetangulia nusu fainali ni za kawaida ambazo hazimpi presha na ndiyo maana anawazia ubingwa na siyo namna ya kuwakabili wapinzani watakaocheza nao fainali.
“Yanga, Azam na Mwadui ni timu za kawaida kwa kiwango tulichokuwa nacho hivi sasa, kama walitufunga ni kipindi ambacho hatukuwa kwenye ubora huu, lakini ninaamini Simba ndiyo mabingwa wa FA mwaka huu,” alisema Mayanja.
Mganda huyo amesema mapumziko ya wiki mbili yamemsaidia kukiimarisha upya kikosi chake na kuwapa ari ya kupambana wachezaji wake, hivyo anaamini watacheza kwa kujituma na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo wa kesho na mingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Amesema kurejea kwa mshambuliaji wake Hamisi Kiiza na beki Hassani Isihaka, nako ni moja ya sababu ambazo zinawafanya kuwa na matumaini ya kufanya vizuri msimu huu kutokana na mchango wa wachezaji hao wanapokuwa uwanjani. Bingwa wa Kombe la FA atawakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF-CC) mwakani.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment