EWURA Yashusha bei za Umeme kwa watumiaji wa Viwango tofauti Kuanzia Leo

Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.

Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama za huduma kwa baadhi ya wateja zimeondolewa.

Bei mpya kwa watumiaji wadogo ni sh.100 kwa uniti, watumiaji wa kati ni sh.292 toka 298 ya zamani.Wafanyabiashara wadogo ni sh. 195 toka sh. 200 ya hapo awali.
Tazama jedwali hili kuona mgawanyo wa bei mpya.

TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment