Akiwa kortini kuhusiana na mauaji hayo, Dube ndipo alipomwaga siri hiyo kwamba ni kweli Rais Banana alikuwa akimlawiti yeye na watu wengine kwa kutumia vitisho vya cheo chake na kwamba pamoja na kuripoti jambo hilo kwa wakubwa kibao, walikuwa wanagwaya kumchukulia hatua kiongozi huyo.
Kwa mujibu wa Dube, ambaye Banana alimpenda alipomwona anacheza soka timu za mitaani na akaamua aajiriwe ikulu, rais huyo alikuwa amebobea katika ulawiti wa wafanyakazi wengi wa kiume wa ikulu, licha ya kuwa na mke na watoto. Hata hivyo, kesi ya Dube ndiyo iliyomtia hatiani Banana.
Dube alisema mahakamani kwamba alikataa mara nyingi kufanya ‘mchezo’ huo na Banana alipoitwa faragha ikulu licha ya vitisho hadi alipomchanganyia madawa kwenye soda ya Fanta na ‘kumfanyizia’ kwa mara ya kwanza.
Tangu hapo vitisho vya Banana vikazidi ikiwa ni pamoja na Dube kufungiwa nyumbani kwake, kuachwa katika safari za nchi za nje na kutishiwa kufukuzwa kazi, mambo yaliyomfanya Dube akubali kuendelea kufanyiwa kitendo hicho hadi ‘alipozomewa’ na konstebo aliyemuua.
Banana aliyezaliwa Machi 5, 1936 na kuwa Rais wa Zimbabwe tangu Aprili 18, 1980 hadi Desemba 31, 1987, akiwa pia msomi mkubwa, alishiriki pia kwa kiwango kikubwa kupigania uhuru wa Zimbabwe hadi alipokamatwa mwaka 1997 kutokana na makosa 11 ya tuhuma za kulawiti.
Akiogopa Rais Robert Mugabe angemshikisha adabu kwa kitendo hicho, Banana alikimbilia Afrika Kusini, lakini marehemu Nelson Mandela akamsihi arudi nyumbani kuikabili adhabu hiyo ambapo aliporejea, Januari 18, 1999, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela ambapo miaka tisa angeitumikia nje ya gereza. Pia mamlaka husika za kidini zilimvua ‘uchungaji’ wake.
Alikaa gerezani miezi sita tu na kuachiliwa Januari 2001.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment