Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watu 63
wanaodhaniwa kuwa majambazi wa kutumia silaha katika operesheni
endelevu ya kuwasaka majambazi wanaofanya matukio mbalimbali.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi
kanda maalumu Simon Sirro aamesema, miongoni mwa majambazi waliokamatwa
ni Ibrahim Juma(31) mkazi wa Kiwalani Kigilagila, Samweli Mbonea (40)
Fundi gereji Mkazi wa Kiwalani pamoja na Anthony Kanywenywe (60)
Mwindaji na mkazi wa Kiwalani.
Amesema
majambazi hao walikutwa na taa kubwa nne za magari, pawa windo moja na
nati za magari na watuhumiwa sita kati ya waliokamatwa wamekiri
kushiriki katika matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha katika maeneo
mbalimbali likiwemo la Riki Hill Hotel katikati ya jiji na Lake oil
Buguruni.
Katika
tukio jingine kikosi maalumu cha kupambana na majambazi kimefanikiwa
kukamata silaha sita aina ya SMG moja ,Short gun pump action tatu na
Rifle mbili katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Amesema
silaha aina ya SMG iliyokatwa kitako ilipatikana baada ya askari
kuwafyatulia risasi majambazi hao waliokuwa eneo la vingunguti ndipo
walipoitupa silaha hiyo ikiwa kwenye mfuko mweusi wa plastiki na wao
kukimbia katika bonde la Mto Msimbazi.
“Tunaendelea
kuwatafuta watuhumiwa hao na upelelezi unaendelea ili kubaini mmiliki
halali wa silaha hiyo. Hatupotayari kuendelea kuona maovu yakiendelea
kufanyika, jeshi lipo imara na tutapambana nao,” alisema Sirro.
Ameongeza
kuwa jeshi hilo pia lilifanikiwa kukamata silaha Rifle mbili katika
eneo la Masaki ambazo zilikuwa zimefichwa na kufunikwa kwa taulo zikiwa
na maandishi ya Collessium Fitness Club moja ikiwa na namba A 6777013
iliyosajiliwa nchini kwa namba TZCAR 58596, na nyingine ikiwa na namba L
691848176 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR 75062.
Wakati
huo huo Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa
kukamata jumla ya risasi 15 za silaha ndogo aina ya bastola zikiwa
kwenye magazine.
Risasi hizo alikutwa nazo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mamboleo Willium (41) Mfanyabiashara mkazi wa Mikocheni.
Katika
mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa na risasi hizo kinyume na sheria
na kushindwa kueleza mahali alipozipata, mtuhumiwa anaendelea
kushikiliwa na uchunguzi unaendelea kufanyika
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment