Je,Wajua? Mchezaji Yeyote Akijiunga na KRC Genk Anapewa Benz, Mbwana SAMATTA Kapewa?! (+Pichaz)


Mastaa wa soka Ulaya kutembelea magari ya kifahari sio ishu mpya sana na unaambiwa asilimia kubwa ya club za soka Ulaya huwa wana mikataba na kampuni za magari kama ilivyo kwa KRC Genk ya Ubelgiji anakocheza Mtanzania Mbwana Samatta ambao wana mkataba na Mercedes Benz.

Hii ni Benz ya Kumordzi
Unaambiwa KRC Genk wana mkataba na Mercedes Benz ambao kila mchezaji wa klabu hiyo huwa anapewa Benz jipya hata kama atapenda kununua gari kutoka katika kampuni nyingine kama ilivyo kwa Leone Bailey ambaye anatembelea Benz na Range Rover.

Kebano Neeskens nyuma ikionekana Benz yake
Mbwana Samatta bado hajapewa Benz yake kwa sababu hakufaulu mtihani wa alama za barabarani kwa kupungukiwa alama nne, kwa sasa anaendeshwa tu na dereva wa klabu anapokwenda sehemu mbalimbali lakini akifaulu mtihani atapewa kibali cha kuendesha gari Ubelgiji.

Mbwana Samatta

Sandy Walsh na gari lake

Leon Bailey anamiliki Range Rover pia licha ya kupewa Benz

Hii ni gari ya nahodha wa KRC Genk Thomas Buffel
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment