Madhehebu ya Kiislam Yaunga Mkono Kasi ya Rais MAGUFULI na Utumbuaji Majipu Uchungu

KASI ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli inazidi kushika moto baada ya Kiongozi Mkuu wa Chuo cha Kiislam (Hawza) Imam Swadiq ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Waislam wa Madhehebu ya Shia Ithnasheria, Tanzania, Shekh Hemed Jalala amewataka Watanzania na waumini wa madhehebu yote nchini kumuunga mkono kwa kasi yake.

Shehe Jalala akizungumza leo na wanahabari katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mmoja wa wanafunzi wa Mtume Mohamed (S.A.W), Imam Ali (A.S), amesema alikuwa kiongozi jasiri, mpenda haki, aliyepinga rushwa, muwajibikaji na mpinga ufisadi, kama ilivyo kwa sasa kwa Rais Magufuli ambaye ameonesha nia ya dhati ya kuifanya Tanzania kuwa mpya kwa kupinga ufisadi, rushwa na mambo mengine ambayo yanawaumiza Watanzania wa hali ya chini.
“Tunaadhimisha zaidi ya miaka 1430 ya kuzaliwa kwake

Imam Ali kwa kuwa alikuwa mwanafunzi bora wa kuigwa kwa kile alichokipigania ndicho kinachoonekana kwa Rais Magufuli, viongozi wa dini tuwaongoze waumini wetu katika kumuombea na kukemea pale tunapoona si sahihi, ila mpaka hapa tulipo ameonesha dira ya Tanzania mpya,” alisema Shehe Jalala.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment