Hayo yameelezwa jana na Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (Dart), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk. Amelisema tayari wamiliki wote wa mabasi walishalipwa fidia ya kubadili njia.
“Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabara kabla ya Mei 10,” amesema Mabrouk.
Mradi wa Dart unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu na tayari mabasi hayo yameshaanza kufanya majaribio katika njia mbali mbali katikati ya jiji huku changamoto kubwa ikidaiwa na waendesha pikipiki, raia na daladala kupita kwenye njia hiyo ya mradi na kusababisha msongamano wa magari kitendo ambacho kinalazimu mabasi hayo nayo kujikuta yakikaa foleni.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment