
ALIYEKUWA kocha wa Chelsea kabla ya
kutimuliwa, Jose Mourinho amekuwa akihusishwa kuhamia klabu ya
Manchester United msimu ujao huku taarifa za wazi zikisema kuwa tayari
ameshasaini mkataba wa awali wa kukinoa kikosi hicho cha Mashetani
Wekundu.
Ripoti kutoka kwenye redio ya Cadena Cope
ya nchini Hispania zinasema kuwa kandarasi ya Mreno huyo kuhamia Man U
imeleta sintofahamu baada ya wamiliki wa klabu hiyo (Familia ya Glazer)
kumgomea kujiunga na Man U.
Kocha huyo mahiri duniani mwenye umri wa miaka 52 amekuwa na
matumaini makubwa ya kuinoa Man U msimu ujao ili kumrithi Louis van Gaal
anayeonekana kushindwa kuimudu klabu hiyo na kufikia malengo yake.

Mourinho aliyewahi kuifundisha Real Madrid alitimuliwa Chelsea
mwanzoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza na nafasi yake kuchukuliwa
na Guus Hiddink kwa muda kabla ya jana kumteua rasmi Antonio Conte kuwa
kocha wao Mkuu.
Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi wa
Man United, Ed Woodward amesema, Van Gaal ana mkataba wa miaka mitatu
klabuni hapo, lakini wapo tayari kumpa muda wa miaka miwili tu kuendelea
kuinoa klabu hiyo na endapo atashindwa kuisaidia kunyakuwa Kombe la
Mabingwa (Champions League) basi atalazimika kuondoka klabuni hapo.
Japo ndani ya Bodi ya Wakurugenzi wa
Klabu ya Manchester United kutofautiana mitazamo kuhusu nani ainoe klabu
yao msimu ujao, Ed Woodward ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho iwapo ni
Mourinho au Van Gaal kuinoa hiyo msimu ujao.
CHANZO NA METRO UK
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment