Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Nyanda za
Juu Kusini limekitoza faini ya shilingi milioni 20 Kiwanda cha Karatasi
Mufindi (MPM) kilichopo kijiji cha Mgololo kata ya Makungu katika
Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa baada ya kushindwa
kufanya maboresho katika mfumo wake wa kuchuja maji taka kabla ya
kuingia kwenye mto licha ya kuagizwa kufanya hivyo mara kadhaa.
Bw.
Godlove Mwamsojo ambaye ni Mratibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini amesema
adhabu hiyo ambayo ni kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya 2014 vifungu
vya 186 na 198 inapaswa kutekelezwa katika kipindi cha siku 14.
Amesema
kiwanda hicho pekee cha uzalishaji wa karatasi nchini kimeshindwa
kudhibiti maji taka yanatoka kiwandani hapo na kutiririshwa katika mto
Kigogo hali ambayo amesema inayaweka rehani maisha ya watu na viumbe
wengine wanaotumia maji ya mto huo.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na
Mazingira, Bw. Luhaga Mpina amewataka wenye viwanda nchini kukidhi
mahitaji ya sheria mbalimbali ikiwemo ya mazingira sambamba na
kuikumbusha NEMC kufanya kazi usiku na mchana bila kuchoka.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment