
Dwight Yorke.
MCHEZAJI wa zamani wa Aston Villa, Dwight Yorke ametangaza rasmi kuwa anahitaji kuwa kocha wa klabu hiyo. Dwight mwenye umri wa miaka 44, hana uzoefu mkubwa katika kufundisha soka lakini anahisi elimu yake ya masuala ya mpira wa miguu na uzoefu wake hasa katika ligi za Uingereza vinamfanya aamani kuwa anauwezo wa kuifundisha Aston Villa.
Ikumbukwe kuwa Dwight aliwahi kuichezea Manchester United na kuwa miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri zaidi katika kutekeleza wajibu wao wawapo uwanjani, pia hakusita kueleza kuwa ana mbinu za aliyekuwa kocha wake, Sir Alex Ferguson hivyo atatumia mbinu hizo kuifikisha mbali zaidi Aston Villa.
‘Nawafahamu vizuri wachezaji, utamaduni na historia ya Aston Villa. lakini cha ziada naifahamu nauelewa mkubwa kuhusu ligi za Uingereza.’
‘Nitaomba hiyo kazi (kazi ya kuifundisha Villa) na nitafanya kama navyoongea sasa. Natumaini watanipa intavyuu nizungumze nao.’ Alisema Dwight.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment