Mmoja wa vijana wanaoosha vioo vya magari katika sehemu za mataa
ya kuongozea magari maeneo ya Kisutu akisafisha kioo cha gari wakati
agizo la Mkuu wa Mkoa, Makonda linamkataza kufanya hivyo.
Kijana (kushoto) akitaharuki baada ya kuona kamera ya paparazi.
Ombaomba hao wakijificha ili wasifotolewe na kamera ya paparazi katika barabara ya Bibi Titi Mohammed Dar.
OMBAOMBA katikati mwa jiji la Dar es
Salaam hii leo wameonekana kumbipu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda baada ya agizo lake alilolitoa mwishoni mwa wiki ikliyopita ya
kuwataka kuondoka mara moja maeneo ya katikati ya jiji hilo kugonga
mwamba.
Mtandao huu umefanikiwa kuwanasa ombaomba hao wakiwa katika Barabara
ya Bibi Titi Mohammed maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiomba
abiria kwenye daladala na waendesha magari madogo pasipo kujali agizo
hilo.
Na Denis Mtima/Gpl
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment