Alizaliwa mwaka 1950 Oct katika mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Msoga katika familia ya kisiasa na kilimo. Baba yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Pangani na babu yake naye ambaye alikuwa ni Chief wa Wakwere, Chief Kikwete.
Alipata elimu ya Msingi Msoga kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Kibaha akiwa pia ni mwenyekiti serikali ya wanafunzi na vijana wa TANU 1966 na Baadaye Tanga school. Ambapo alijiunga na chuo kikuu Dar es salaam, ambapo pia alikuwa mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi na kuhitimu Shahada ya uchumi 1975 alipojiunga na Jeshi.
Aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida 1977 na baadae kuhamishiwa Zanzibar kwa kazi maalum baada ya muungano wa TANU na ASP mpaka kufikia mwaka 1980 aliporudishwa makao makuu ya chama (CCM).
Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa mbunge na pia NaibuWaziri wa Nishati na Madini chini ya uongozi wa MH. Al Ahsan Mwinyi mpaka kufikia mwaka 1990 ambapo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa maji nishati na madini.
Mwaka 1994 aliteuliwa kuwa waziri wa uchumi akiwa na umri wa miaka 44 ambapo alikuwa ni waziri mwenye umri mdogo kuwahi kuteuliwa. Kufika mwaka 1995 alitueliwa kuwa waziri wa mambo ya nje chini ya uongozi wa Rais Benjamin W. Mkapa na kuongoza wizara hiyo kwa miaka 10 mpaka kufikia mwaka 2005 ambapo alichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.
Katika Nyanja za kimataifa Mh. Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wanadiplomasia ambae amefanya mambo mengi katika bara la Afrika na Dunia, kama vile kutatua migogoro katika nchi za maziwa makuu, jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa kama Mwenyekiti wake (EAC) baadhi ya mambo ambayo dunia inampongeza ni pamoja na Mwaka 2005 akiwa kama Mwenyekiti mwenza wa mikutano wa Helsinki (Helisinki process on Globalization and Democracy) aliweza kuongoza mikutano huo kwa mafanikio makubwa.
2013 akiwa ndiye kiongozi pekee kutoka Afrika aliyeshiriki katika mkutano nchi za umoja wa Ulaya EU wa Alpbach Austria aliliwakilisha bara la Afrika vyema katika kutafuta fursa za maendeleo na ushirikiano kimataifa.
Dr. Jakaya Kikwete pia amekuwa Mjumbe tume ya Elimu Duniani ikiongozwa na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown katika kutafuta namna ya kugharamia Elimu duniani (TICFGEO) kwa mwaka 2015.
Kwa mwaka huu 2016 Dr. Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa Mjumbe wa kamati ya Amani nchini Libya katika kusaidia kurudisha amani nchini Libya
Pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mwenza kwa tume ya kusaidia afya ya Mama na motto duniani kwa mwaka huu 2016 ikiwa ni katika jitihada zake kuhakikisha Afya na mama na motto duniani kote zinalindwa.
Kwa mtazamo huo nina imani kubwa kwa kipindi ambacho Mh. Ban Ki-Moon ataachia ofisi, Mwanadiplomasia huyu ndiye atakayechukua viatu vyake .
Hizi ni baadhi ya tuzo za heshima alizowahi kupata toka nchi mbalimbali
2007: Sullivan Honor
2007: The AAI African National Achievement Award (on behalf of Tanzania).
2009: US Doctors for Africa Award.
2011: Social Good Award from the United Nations Foundation
2011: South-South Award for Global Health, Technology and Development
2012: FANRPAN Policy Leadership Award from the Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network.
2013: Africa's Most Impactful Leader of the Year by the Africa Leadership Magazine
2013: ICCF Mengha Award by the International Conservation Caucus Foundation
2014: Icon of Democracy Award, from The Voice Magazine (Netherlands)
2015: Leadership Excellence Award by the Pan-African Youth Union.
2015: African Achievers Award by the Institute for Good Governance in Africa.
2015: African Statesman of the Year by the The African Sun Times.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment