Wafanyabiashara wawili raia wa China wamepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu shtaka la kuuza bidhaa bila kutoa
stakabadhi za kodi za kieletroniki (EFD).
Washtakiwa hao ni
Paishu Chea na Apple Chen ambao wote walisomewa mashtaka yao kwa
mahakimu wawili tofauti na kulikiri kutenda makosa, hivyo kulipa faini
ya Sh2 milioni kila mmoja ili kuepuka kifungo cha miaka mitatu.
Katika
kesi ya kwanza, Mwendesha Mashtaka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Noah Tito alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa mahakama
hiyo, Saidi Mkasiwa kuwa kati ya Machi 14 na 16 katika Mtaa wa
Narung’ombe na Kongo, Chea aliuza bidhaa za thamani ya Sh28,000 bila
kutoa risiti ya EFD kinyume na sheria.
Katika kesi ya pili,
Wakili wa TRA, Consolatha Andrew alidai Cheng alitenda kosa la kutotoa
risiti kati ya Machi 14 na 15 katika Mtaa wa Narung’ombe na Kongo.
Andrew
alidai Cheng ambaye ni mfanyakazi katika Kampuni ya Dong Shen
International aliuza viatu vyenye thamani ya Sh1.4 milioni, lakini
hakutoa risiti kwa mnunuzi kama sheria inavyomtaka.
Hakimu wa mahakama
hiyo, Flora Haule alimuamuru mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh2 milioni
au kwenda jela miaka mitatu. Hata hivyo mshtakiwa alilipa faini.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment