Wakati sakata la Kampuni ya Lugumi
kudaiwa kushindwa kutekeleza mradi wa utambuzi wa vidole kwenye vituo
vya polisi likianza kudaliwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga amesema hana uhusiano wowote na kampuni hiyo kama watu
wanavyodai.
Kitwanga ambaye alihusishwa na Lugumi kupitia kampuni ya
Infosys iliyodaiwa kwamba kiongozi huyo ni mmoja wa wanahisa wakati
akiwa mfanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ameeleza kuwa hahusiki
na wala halijui suala la Lugumi.
Infosys ambayo imekanusha kuhusika
katika sakata hilo imedaiwa kuwa iliisaidia kampuni ya Lugumi kupata
vifaa kutoka kampuni ya Dell ya Marekani ili viweze kufungwa kwenye
vituo vya polisi.
Jana Kitwanga alisema
anashangazwa jinsi anavyohusishwa kwa maelezo kuwa wakati tukio hilo
likitokea mwaka 2011, yeye hakuwa waziri wa wizara hiyo.
“Inanishangaza
sana sihusiki na wala silijui hili suala la Lugumi. Wakati linatokea
sikuwa waziri wa wizara hii ndiyo maana huwa sipendi na wala sitaki
kuzungumza chochote kuhusu Lugumi,” alisema.
Kitwanga alifafanua kuwa
baadhi ya mambo yameanza kubainika baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, licha ya kutotaka kuweka wazi kama suala la
Lugumi ni miongoni mwa mambo hayo.
Kampuni ya Lugumi ilibainika kutotimiza
matakwa ya mkataba wake baada ya kufunga mashine 14 tu kati ya 108 zilizotakiwa kufungwa,
licha ya kulipwa zaidi ya asilimia 90 ya fedha kwa mujibu wa mkataba.
Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) ya mwaka 2013/14
ndiyo iliyofichua udhaifu huo.
Utekelezwaji wa mkataba huyo uliwasilishwa jana kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na
mwenyekiti wake Aeshi Hilaly alisema wameanza kuupitia na
watakapokamilisha wataweka kila kitu wazi.
Kwa upande wake Ndugai alipotakiwa kuzungumzia suala
hilo alisema, “Mimi sijapata taarifa zozote za Lugumi. Jambo hilo bado
lipo katika kamati ya bunge.”
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment