Yanga iliyolazimishwa sare ya 1-1 na Ahly inatarajia kurudiana na wapinzani wao hao Jumatano usiku kwenye uwanja wa Borg el Arab, mjini Alexandria.
Iwapo itafanikiwa kuitoa timu hiyo itasonga mbele kwa hatua nyingine.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema baada ya mchezo huo wataanza safari yao usiku wakiwa na matumaini ya kwenda kufanya vizuri.
“Tunaanza maandalizi ya kwenda kushinda, baada tu ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar tutaondoka na tuna kila sababu ya kushinda kwani mwalimu anafanyia kazi mapungufu machache yaliyoonekana katika mchezo wetu wa kwanza,” alisema.
Licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm alisema hawajakata tamaa, kwani katika soka lolote linaweza kutokea na kuwatoa waarabu hao.
Pluijm alisema ameiona Al Ahly vizuri na kuahidi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza yasijirudie tena katika mchezo huo wa ugenini. Kocha huyo Mholanzi alisema inawezekana kuwatoa Waarabu kama wachezaji wake watafanya kazi kama anavyowaelekeza.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment