BUNGE LAINGILIA KATI MKATABA TATA WA JESHI WENYE THAMANI YA BILIONI 37

BUNGE limetoa siku tatu kwa Jeshi la Polisi kuwasilisha kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mkataba wa Kampuni Lugumi Enterprises wenye thamani ya Sh bilioni 37.

Hatua hii inakuja siku mbili baada ya jeshi hilo kudaiwa kukaidi agizo la kamati hiyo, iliyotaka likabidhi nyaraka za utekelezaji wa mkataba ufanyiwe tathmini kutokana na malalamiko yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG) katika hesabu za mwaka 2013/2014.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Aeshi Hilaly alisema agizo la kamati la kutaka mkataba huo, lilitolewa wiki iliyopita kuwezesha wabunge kuangalia utekelezaji wake.
“Jana (juzi) ilikuwa siku ya mwisho kwa jeshi kuwasilisha mkataba huo ofisi za Bunge, lakini mpaka leo (jana) muda huu ninapozungumza nanyi (saa 7:30 mchana) walikuwa hawajawasilisha. “

Siku zote tumekuwa tukitoa maagizo kwa mdomo na taasisi nyingi zimekuwa zikitekeleza, lakini hili la mkataba wa Lugumi naona kwa wenzetu limekuwa gumu, hivyo tumeamua kuwakumbusha kwa maandishi,” alisema.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment