CCM ARUSHA WALIA NA HUJUMA HIZI KUTOKA CHADEMA

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha, Michael Lekule Laizer amemuonya Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Mosses Mabula kushiriki vitendo vya hujuma katika halmashauri hiyo.

Baadhi ya hujuma hizo zinazodaiwa kufanywa na halmashauri hiyo inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni pamoja na kuzinyima miradi kata zinazoongozwa na madiwani wa CCM.

Laizer ametoa tahadhari hiyo mjini hapa jana katika kata ya Mangola Barazani alipokuwa akizungumza katika mkutano wa ndani na viongozi wa chama wa ngazi za matawi na kata kuhusu kero mbalimbali za wananchi wa kata hiyo.

Mwenyekiti huyo alifikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa diwani wa kata hiyo kupitia CCM, Lazaro Emanuel
Emanuel alisema kwa kipindi kirefu tangu ameingia madarakani amekuwa akikosa ushirikiano kutoka kwa uongozi wa halmashauri hiyo akiwepo pia mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Mabula na hadi sasa hajakubaliwa ombi la mradi hata mmoja.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment