Gari lilivyokuwa kwa ndani baada ya kuwaka motoAskari wa Kikosi Maalum cha Zima Moto pamoja mashuhuda wa tukio hilo.Gari lilivyowaka.MashuhudaMashuhuda.
Dereva wa gari hilo, Michael Augustino akitoa taarifa kwa bosi wake.
MOROGORO: Dereva wa gari dogo la
mizigo aina ya lsuzu Carry (Kirikuu) lenye namba za usajiri T 609 CKW,
amenusurika kifo baada ya gari hilo alilokuwa akiendesha kuwaka moto
katika eneo la Masika katikati ya Mji wa Morogoro, leo
Wakizungumza na mwanahabari wetu aliyefika eneo la tukio, mashuhuda wa tukio hilo Bernard Joseph na Juma ldd walisema;
“Huyu dereva wa kirikuu alikuwa akitokea
eneo la Msamvu (Kituo Kikuu cha Mabasi Yaendayo Mikoani) alipofika hapa
Masika jirani na ‘round about’ tulishuhuida gari lake likiwaka
moto kwa nyuma na yeye hakuwa na habari aliendelea na safari hivyo boda
boda mmoja aliamua kuwasha pikipiki yake na kumkimbilia na kumjulisha
tukio hilo ambapo alisimama na kushuhudia gari hilo likiendele kuwaka
moto,” walisema mashuhuda hao
Kwa upande wake dereva wa gari hilo aliyejitambulisha kwa jina la Michael Augustino alisema.
“Nashangaa sana huu moto ulikotokea,
gari hili injini iko mbele iweje moto utokee huku nyuma ambako hakuna
kitu chochote na kama unavyoona sikuwa na mzigo wowote ndani ya gari na
washukuru hawa boda boda wa hapa Masika wamenikimbilia na kunipa taarifa
za moto huo, vinginevyo ungefika huku mbele kiwa kwenye mwendo wa kasi
nahisi milango ingeji-lock na mimi ningeuungua vibaya,”
“Namshukuru Mungu kwa hili”alisema Agostino huku akipiga simu kwa mmiliki wa gari hilo.” Alisema Michael.
Askali wa Kikosi Maalum cha Zima moto,
mwenye cheo cha nyota Moja akimhoji dereva wa gari hilo huku wakikagua
kifaa maalumu cha kuzima moto kilichokuwa ndani ya gari hilo.
Picha zote na Dustan Shekidele, Morogoro -GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment