Kamati
ya kudumu ya Bunge inayoshughulikia Hesabu za Serikali (PAC) imeunda
kamati ndogo ya watu tisa itakayochunguza kwa kina mkataba uliozua utata
wa Sh37bilioni ulioingiwa baina ya Jeshi la Polisi na Lugumi
Enterprises.
Pande
hizo mbili, Jeshi la Polisi na Lugumi Enterprises, ziliingia mkataba
huo kwa ajili ya kufunga vifaa 108 vya kuhifadhia alama za vidole katika
vituo vya polisi.
Akizungumza
na wanahabari leo mjini Dodoma, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Aeshi
Hilary amesema kamati hiyo itafanya kazi kwa siku 30, kuanzia Jumatatu
ijayo.
Wajumbe
tisa wa kamati hiyo ndogo ni; Japhet Hasunga (Vwawa-CCM), wengine wa
CCM ni Livingstone Lusinde (Mtera), Stanslaus Mabula (Nyamagana), Haji
Mponda (Malinyi) na Hafidh Ali Tahir (Dimani).
Wabunge
wa upinzani waliopo katika kamati hiyo ni Nahenjwa Kaboyoka (Same
Mashariki-Chadema), Musa Mbaruk (Tanga Mjini-CUF), Tuza Malapo (Viti
Maalum-Chadema) na Khadija Nassor Ali (Viti Maalum-CUF).
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment