Mkuu
wa mkoa wa MWANZA John Mongella (pichani) ametoa saa 24 kwa kamanda wa
Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi
kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba
kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uaandaji wa malipo ya
Halmashauri (EPICOR)
Mhe.
Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha
kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo
taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa
kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo
mbali mbali ya halmashauri.
“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana",
amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza
kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo.
Akizungumza
kando ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri, kaimu mhazini wa
halmashauri hiyo Baraka Munuo, alidai kupokea taarifa za kupotea kwa
Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe
akimuelezea upotevu huo.
Katika
hatua nyingine mkuu wa mkoa wa MWANZA, amemuagiza mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya ukerewe,, kupitia mafaili na kubaini watumishi
waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo mkuu wa
mkoa amedai linachangia watumishi kufanyakazi kwa mazoea.
”Mkurugenzi
nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika
kituo hiki kwa muda mrefu. Haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na
moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana"
alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama
kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.
Awali
akisoma taarifa ya wilaya hiyo, mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph
Mkirikiti,alimwambia mkuu wa mkoa kuwa hali ya ulinzi na usalama ni
shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo huku akisema
wilaya imefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kilicho kuwa
kimepiga kambi katika Wilaya hiyo kwa zaidi ya miezi 6.
Mkuu
wa mkoa wa yupo katika ziara yakujitambulisha na hii ikiwa ni wilaya
yake ya saba,Mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi, Magu,
Nyamagana, Ilemela na Kwimba na hii ya Ukerewe inakuwa wilaya ya saba
huku akiwa amebakiza wilaya moja ya Sengerema yenye halmashauri za
Buchosa na Sengerema yenyewe.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment