Kikosi cha Uokoaji kikiopoa mwili wa mmoja wa watu waliokuwa kwenye gari hilo.
WATU wawili wanasadikiwa kufariki dunia baada ya gari
aina ya Toyota Hiace walilokuwemo kuserereka wakati likiingia katika
kivuko na kutumbukia baharini leo eneo la Kivukoni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa mkuu wa kikosi cha Uokoaji
cha Zimamoto, tayari mwili wa mtu mmoja mwanaume umepatikana na jitihada
za kusaka mwili wa mtu mwingine anayesadikika kuwa ni mwanamke
zinaendelea.

Zoezi la uokoaji likiendelea.
Mashuhuda wa ajali hiyo wanaeleza kuwa chanzo cha gari hiyo kuingia
na kuzama baharini kimetokana na kile kinachodaiwa kufeli kwa breki
wakati dereva wa gari hiyo akikata kona kuelekea upande wa mbele ambapo
gari zenye uharaka zinapewa nafasi kukaa mbele pindi kivuko kitakapofika
ziwe za kwanza kuingia katika kivuko hicho.

Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kikiwa eneo la tukio.
Kaka ambaye ni manusura wa ajali hiyo anasema, ndugu hao
waliotumbukia kwenye gari akiwemo dada yake ambaye bado jitihada za
kumtafuta zinaendelea kwa pamoja walikuwa wakitokea mkoani Mbeya kwenye
msiba.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment