Alisema, mita hizo mpya zitaiwezesha mamlaka hiyo kupata vipimo sahihi vya mafuta na kukusanya mapato yanayostahili, kulingana na mafuta yaliyopo.
Akizungumza alipofanya ziara kukagua mita hizo zinazojengwa Kigamboni, Dar es Salaam, Profesa Mbarawa alisema kuwa zimekwishaanza kufanyiwa majaribio na zitaanza kufanya kazi Mei. “Nawaagiza muajiri wataalamu wa kusimamia hizi mita ili kuziwezesha kufanya kazi kikamilifu. Ujenzi wake unagharimu Sh bil 12,” alisema Profesa Mbarawa.
Alitembea daraja jipya la Kigamboni aliloeleza kuwa litazinduliwa Aprili 16, mwaka huu na Rais John Magufuli na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kutoharibu miundombinu ya daraja hilo. Katika hatua nyingine, Mbarawa alitembelea eneo la kusafirishia mizigo inayokwenda Zanzibar na kuagiza mazingira ya kazi ya eneo hilo yaboreshwe.
Pia, alisisitiza umuhimu wa kuboresha huduma za benki ili kuondoa adha ya wafanyabiashara kusafiri na fedha kwa umbali mrefu kwani ni hatari kwa usalama wao. “Mamlaka ya Bandari inatakiwa kuweka mifumo ya kielektroniki katika utendaji kazi zake, acheni kutumia karatasi,” alisema.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment