Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), Luhaga
Mpina amekiamuru Kiwanda cha Serengeti Breweries Limited (SBL), kulipa
faini ya Sh16 milioni kwa kosa la kutiririsha maji yasiyo salama kwenye
makazi ya watu.
Uamuzi huo ulichukuliwa mwishoni mwa wiki
iliyopita mbele ya baadhi ya viongozi wa SBL kilichopo Chang’ombe
Manispaa ya Temeke na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (Nemc), baada ya kujiridhisha kuwa kilikiuka taratibu za
utunzaji mazingira na kutotekeleza amri halali kwa zaidi ya miaka
miwili.
Mpina aliigiza kiwanda hicho, kulipa faini ndani ya siku
saba na kwamba asieleweke vibaya kuhusu uamuzi huo, bali anasimamia
sheria.
“Nasimamia sheria wala sina nia mbaya na kiwanda chenu, naomba nieleweke hivyo na faini hii mlipe kwa wakati,” alisema Mpina.
Mkurugenzi
Mkuu wa Nemc, Bonaventure Baya alisema baraza hilo limejijengea
utaratibu wa mara kwa mara kufuatilia kanuni za afya za kiwanda hicho
hasa majitaka yanayotiririka kuelekea kwenye makazi ya watu.
Meneja
Mhandisi Biashara wa SBL, Peter Mkongwa alikanusha tuhuma hizo na
kwamba, maji hutibiwa kwa dawa kabla ya kutiririshwa katika makazi ya
watu. Alisema: “Tunasubiri mashine maalumu ya kuvuta maji hayo ili
yaingie katika bomba.”
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment