Shirikisho la soka Tanzania TFF
leo May 26 2016 limetangaza maamuzi yake kuhusu zile habari zilizokuwa
zinatarajiwa na wengi kuwa litaandaa michuano ya klabu Bingwa Afrika
Mashariki na kati kwa mwaka 2016 baada ya Zanzibar kushindwa kuandaa michuano hiyo.
Sababu kubwa za TFF kushindwa kuandaa michuano hiyo ambayo maarufu kama Kombe la Kagame ni kutokana na kubanwa na ratiba ya kitaifa na kimataifa, kutokana na Yanga
kushiriki katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika, hivyo
ratiba zitaingiliana na michuano hiyo iliyokuwa imepangwa ichezwe June
na July.
IMETOLEWA NA TFF: tff.or.tz
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment