Serikali Yazidiwa Mzigo wa Vijana Wanaotakiwa Kujiunga JKT

VIJANA wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa mujibu wa sheria wamekuwa wengi kiasi cha kuifanya Serikali kushindwa kuwachukua wote, Bunge limeelezwa.

Hivyo, kutokana na sababu hiyo, Serikali imeamua kuongeza idadi ya kambi za mafunzo ili wachukuliwe wote. Hayo yalisemwa bungeni jana mjini hapa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Munira Mustafa Khatib (CCM) aliyetaka kufahamu ni kwa nini Serikali isianzishe mpango maalumu wa kuwapeleka JKT vijana wanaomaliza kidato cha nne.

Akijibu swali hilo, Waziri Mwinyi alisema, “Uwezo wa JKT kwa sasa kuchukua vijana wa kujitolea ni kati ya vijana 5,000 hadi 7,000 kwa mwaka kutokana na bajeti inayotolewa.
Alisema, utaratibu wa sasa wa vijana kujiunga na JKT ni ule wa kujitolea kwa vijana wenye elimu ya kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu na ule wa mujibu wa sheria unaowahusu waliomaliza kidato cha sita.

“Kuwachukua vijana wote wanaomaliza kidato cha nne kama anavyoshauri mbunge hautowezekana kutokana na uwezo mdogo kifedha,” alisema.

Hata hivyo, alisema ushauri huo ni mzuri na serikali itafanya maandalizi ya kambi nyingi zaidi na kutenga bajeti kubwa zaidi kwa ajili ya uendeshaji kwa kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment