Bado ajali za barabarani zimezidi kuongezeka kila kukicha, baada ya July 4 2016 taarifa za mabasi mawaili ya kampuni moja ya City Boys kupata ajali kwa kugongana uso kwa uso maeneo ya Maweni Singida, leo July 5 zimetoka taarifa za mwanasoka Tanzania kupata ajali ya gari.
Kupitia account ya instagram ya klabu ya Kagera Sugar ya Bukoba, imetoa taarifa za mchezaji na nahodha wake wa zamani Maregesi Mwangwa kupata ajali ya gari, katika taarifa hiyo ya Kagera Sugar imeeleza kwa ufupi kuwa mchezaji huyo kapata ajali, lakini hali yake inaendelea vizuri.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Maregesi Mwangwa alikuwa nahodha wa klabu ya Kagera Sugar, lakini alihama klabu hiyo June 2015 na kujiunga na klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga, kandiliyetu.com bado inafutilia kwa kina chanzo cha ajali na eneo alilopata ajali mchezaji huyo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment