VIDEO: Neymar Alivyoiongoza Brazil Kushinda Medali ya Dhahabu Olympic Katika Soka


Wakati Ligi Kuu mbambali dunia zikiendelea August 20 2016, katika uwanja wa Maracana Rio de Janeiro Brazil timu ya taifa ya nchi hiyo inayoshiriki Olympic ilicheza mchezo wa fainali ya Olympic dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani, huu ulikuwa ni mchezo ambao ulihudhuriwa na mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt.

Neymar do Santos amefanikiwa kuiongoza timu yake ya taifa kutwaa medali ya dhahabu ya kwanza katika historia ya mashindano ya Olympic kwa mchezo wa mpira wa miguu, ushindi huo dhidi ya Ujerumani utafsirika kama ni kisasi kwa kutokana na kuwahi kufungwa 7-1 miaka miwili iliyopita katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la dunia.

Brazil ambao wamewahi kutwaa mataji mengi ya soka wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa penati 5-4 hiyo ni baada ya mchezo kumalizika katika muda wa kawaida wakiwa sare ya goli 1-1, magoli ambayo yalifungwa na Neymar dakika ya 26 na kwa upande wa Ujerumani Max Meyer dakika ya 59, Brazil wamewahi kuikosa medali ya dhahabu ya Olympic katika vipindi vitano tofauti.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment