JESHI
la Polisi katika Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya mkoani Mara, linawasaka
watuhumiwa watano wanaotajwa kuhusika kubaka wasichana wawili katika
eneo hilo.
Kamanda
wa Polisi wa kanda hiyo, Andrew Satta alisema, watu hao wanatuhumiwa
kuwabaka wasichana hao katika matukio mawili tofauti yaliyotendwa kwa
nyakati tofauti Machi 26, mwaka huu katika wilaya za Rorya na Tarime.
Satta
alisema kuwa, katika tukio la kwanza mwanafunzi wa shule ya msingi
Kibasisi iliyopo kwenye kijiji cha Kangariani wilayani Tarime (Jina
limehifadhiwa), alibakwa na watu wawili wakati akirejea nyumbani kutoka
shuleni siku hiyo ya Machi 26.
Kamanda
Satta alisema kuwa, mwanafunzi huyo alikutana njiani na watu wawili
waliokuwa wamejifunga vitambaa vyeusi usoni, ambao walimkamata kwa
nguvu, kumburuza vichakani na kumbaka kwa zamu. Alieleza zaidi kuwa,
baada ya kumbaka, watu hao walimdhibiti asipige kelele kwa kumfunga
kitambaa mdomoni.
“Walipomaliza kumbaka walitokomea kwenye vichaka na kutorokea mahali pasipojulikana, lakini Polisi inawasaka,” alisema na kuongeza kuwa, tukio hilo liliripotiwa Polisi na mwanafunzi huyo.
Katika
tukio la pili, Kamanda Satta alisema kuwa, siku hiyo usiku kwenye
kijiji cha Ruhu kwenye mwalo wa wavuvi wilayani Rorya, msichana mwenye
umri wa miaka 21 (Jina limehifadhiwa), alidanganywa na vijana wanne kuwa
aliitwa na rafiki yake wa kiume, jambo lililomfanya awaombe
wamsindikize alipo na walitii.
Kamanda
Satta alisema kuwa, bila kujua nia ya vijana hao kumdanganya hivyo,
binti huyo ambaye hata hivyo anawatambua na kufahamu majina yao,
alikubali na kuondoka nao.
Alisema
kuwa baada ya kufika kwenye eneo la mwalo wa wavuvi, karibu na vichaka,
huku kukiwa na giza nene, waliamua kumkamata kwa nguvu na kumfunga
mdomo kwa kitambaa asiweze kupiga kelele.
“Walipofanikiwa
kudhibiti asipige kelele vijana hao wanne walimbaka kwa zamu na
kumwacha akiwa hoi vichakani, ndipo binti huyo alipoamua kujikongoja
hadi kwenye eneo alipopata msaada wa wasamaria waliomsindikiza kutoa
taarifa kwenye kituo cha Polisi na kwenda hospitali kwa matibabu”, alisema.
Watu
hao waliotajwa na binti huyo kuwa ndio waliombaka ni pamoja na Ophia
Robert ambaye amekamatwa, Nchama Bureki, Robert Shija na mwingine
aliyetajwa kwa jina moja, Mashije.
Aliwaonya
wanaoendeleza ubakaji katika kanda hiyo kuacha kwa sababu msako
unaofanywa ni endelevu na jeshi hilo halitasita kuwachukulia hatua za
kisheria.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment