Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.
MUSA MATEJA, amani
DAR ES SALAAM: Wakati msuguano mkubwa ukiwa umeibuka,
Mbongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akisukuma madongo kwa Magazeti
Pendwa ya Global Publishers kwamba yanamtungia uongo kuhusu hali yake ya
kurejea kubwia unga akisema hayuko hivyo kwa sasa, kuna taarifa kwamba,
Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ amemuonya kuhusu kutozingatia
matumizi ya dawa za methadone.
Methadone ni dawa zinazotumiwa na waathirika wa matumizi ya madawa ya
kulevya ‘unga’ ambapo Ray C anatumia kwenye Hospitali ya Mwananyamala,
Dar baada ya kuathirika.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini hospitalini hapo, Ray C alipata
onyo hilo baada ya Magazeti ya Global kuandika kwamba nyota huyo
amerejea kwenye kubwia unga huku akiendelea na methadone, hali
‘inayomzimisha’ mara kwa mara.
“Jamani nataka kuwaambia, mnajua mlipoandika kwamba Ray C karejea
kwenye unga wakati akiendelea kutumia methadone, JK alisoma, akamtumia
ujumbe akimtaka ajiangalie kwenye kukazana kutumia dawa na kuachana moja
kwa moja na matumizi ya unga.
“JK amemtaka aangalie mwenendo wake kwa sasa. Yaani bwana sijui vipi, JK anamtakia mema lakini yeye hajijui tu.
“Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba juzikati Ray C alikuja pale
Hospitali ya Mwananyamala (jijini Dar), akawaangukia madaktari wake
wanaomtibu akiwaomba msamaha kwamba amekuwa akiwapuuza katika ushauri
lakini amegundua wao ndiyo msaada mkubwa kwake,” kilisema chanzo hicho.
Mbongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Kitendo hicho kinatokana na madaktari hao siku za karibuni kumshindwa
staa huyo katika kumpa mwongozo wa matumizi ya dawa hizo, hivyo kuamua
kumrudisha nyumbani kwao, Bunju, Dar (habari hiyo iliandikwa na gazeti
hili).
Taarifa zaidi zinasema kuwa pia baada ya Magazeti ya Global kuandika habari ya anayemmaliza Ray C ni kijana Frank, ndugu zake wamemfuata na kumrudisha nyumbani kwao, Arusha.
Taarifa zaidi zinasema kuwa pia baada ya Magazeti ya Global kuandika habari ya anayemmaliza Ray C ni kijana Frank, ndugu zake wamemfuata na kumrudisha nyumbani kwao, Arusha.
“Unajua ndugu zake walikuwa wakimtafuta, alipotoka kwenye gazeti wakamwona, wakamfuata Mwananyamala kumchukua,” kilisema chanzo.
Utafiti uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa ile ‘posti’ ya Ray C
aliyoitupia kwenye mtandao wake wa Instagram mara baada ya kuandikwa na
Gazeti la Ijumaa Wikienda la Machi 28, mwaka huu, habari ikiwa na
kichwa; RAY C ANASWA AMEZIMIKA, akitoa shutuma nzito kwamba picha zile
si zake bali ziliungwaungwa, ameifuta!
Udadisi zaidi unasema kuwa kufutwa kwa posti hiyo kunatokana na Mbongo
Fleva huyo kuguswa na dhamira yake huku pia michango ya wafuasi wake
waliojitokeza kumwandikia ukweli kumwambia, picha zile ni yeye na hakuna
aliyeziunga!
Ray C alipotafutwa juzi ili kujibu madai hayo alikosekana hewani licha ya kupigiwa simu mara kwa mara kwa siku nzima.
Ray C alipotafutwa juzi ili kujibu madai hayo alikosekana hewani licha ya kupigiwa simu mara kwa mara kwa siku nzima.
-via GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment