Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Daraja
la kigamboni litaanza kutumika siku ya Jumamosi tarehe 16, Aprili, 2016
kuanzia saa 12:00 asubuhi.
Katika
siku za mwanzo, magari yatapita bila kulipia tozo hadi Serikali
itakapokamilisha taratibu na kutangaza utaratibu wa kulipia.
Aidha,
watembea kwa miguu na waendesha baiskeli watavuka bure katika Daraja la
Kigamboni. Hata hivyo maguta na mikokoteni haitaruhusiwa kutumia
daraja hilo kutokana na sababu za kiusalama.
Magari
yatakayoruhusiwa kupita katika Daraja la Kigamboni katika siku hizo za
mwanzo ni yale yenye uzito usiozidi tani 10, hatua ambayo itasaidia
kufuatilia mwenendo wa upitaji wa magari katika daraja, barabara za juu
(Interchange) katika eneo la Kurasini, pamoja na kuhakikisha kwamba
magari yanayotoka au kuingia katika daraja hayasababishi msongamano wa
magari katika Barabara ya Nelson Mandela, Barabara ya Kilwa na maeneo
mengine ya jiji.
Baada ya utaratibu kukamilika magari ya aina zote yenye uzito unaoruhusiwa kisheria yataruhusiwa kupita katika daraja.
Mambo muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia ni:-
1)
Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na kufuata
mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu
miundombinu ya daraja
2) Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘Interchange’ ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.
3)
Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango (Toll Gates) ya Kituo cha
kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya kituo
hicho.
4)
Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha uharibifu wa
aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au kuchukuliwa
hatua nyingine za kisheria.
5) Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka katika eneo la daraja.
Aidha,
Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataka madereva wa magari
ya mizigo wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela wakisubiri
kuingia bandarini watafute eneo stahiki la maegesho na kuyaondoa magari
hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoenda kinyume
na agizo hili.
Msongamano wa magari hayo husababisha uharibifu wa barabara na usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara katika eneo hilo.
Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
14 Aprili, 2016
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment