Mtandao wa Madeni na Maendeleo
Tanzania (TCDD) umeitaka Serikali kutafakari upya Sheria ya Asasi za
Kiraia ili kuyaondolea mzigo wa uendeshaji Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali (NGOs) badala ya kuyafungia kutokana na sababu mbalimbali.
Hivi karibuni Serikali kupitia kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali, ilifuta usajili wa NGO’s 110 kwa kuendesha shughuli zao
kinyume cha Sheria ya NGOs Na 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
mwaka 2005.
Kwa mujibu wa msajili huyo, mashirika hayo ni yale ambayo
hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa kipindi cha miaka miwili bila kutoa
sababu za msingi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCDD, Hebron Mwakagenda alisema kuna
haja kwa Serikali kuangalia mashirika hayo kabla ya kukimbilia
kuyafungia.
Aliiomba Serikali ifute ada ya mwaka na ilipwe wakati wa
kusajili tu na aliikosoa pia sheria hiyo akisema inayalazimisha
mashirika hayo kupeleka taarifa zao Dar es Salaam kutoka kila kona ya
nchi badala ya kupeleka kwenye ngazi za wilaya.
“Maofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri za wilaya
ambao pia ni wasajili wasaidizi na waratibu wa shughuli hizi wapewe
mamlaka ya kupokea taarifa za utendaji kila mwaka kwa niaba ya msajili ili kuepusha usumbufu wa kusafiri hadi Dar es Salaam.”
Alisema Hebron Mwakagenda
Edmund Simon wa asasi ya
Umoja wa Wawezeshaji kutoka Kigoma iliyo chini ya mtandao huo,
alisema Serikali inapaswa kuzisaidia NGOs na asasi badala ya
kuzikandamiza.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment