Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella ameuagiza uongozi wa Jiji la Mwanza
kuhakikisha linakabidhi kiwanja namba 28-A kilichopo katika eneo la
Bugando ifikapo Aprili 25, 2016 kwa mmiliki halali wa kiwanja hicho
bwana Justine Eminoga ambacho amekuwa akikidai kutoka kwa mfanyabiashara
wa Jijini humo kwa zaidi ya miaka sita sasa.
Mongella
amefikia hatua hiyo mara baada yakupokea malalamiko kutoka kwa bwana
Justine ambaye alifika katika Jiji la Mwanza kwa ajili kufatilia suala
lake ambalo limedumu kwa zaidi ya miaka sita sasa. Akitoa malalamiko
yake mbele ya mkuu huyo wa mkoa, bwana Justine alidai kuzulumiwa kiwanja
hicho na mfanyabiashara aliye mtaja kwa jina Shanif Mansour ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Kwimba.
Katika
hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametoa siku saba kwa halmashauri za
mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuhakiki watumishi,
ili kubaini endapo kuna watumishi hewa waliosalia katika zoezi la awali,
zoezi la sasa ambalo linasimamiwa na Ofisi ya katibu Tawala wa Mkoa wa
Mwanza kwa kamati maalumu zilizo undwa na mkuu wa Mkoa huo,
Akiwa
katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa aliagiza kukamatwa kwa Afisa
Utumishi msaidizi wa jiji la Mwanza Henry Sedetale, ambaye alisaidia
watumishi hewa watano kuchukua mikopo ya zaidi ya Mil.90 kutoka katika
benki tofauti tofauti, hata hivyo taarifa kutoka Taasisi yakupambana na
kuzuia rushwa mkoani Mwanza iliyotolewa wakati wa kikao hicho na mkuu
wa Takukuru mkoani humo, ilisema mtuhumiwa huyo tayari alikuwa ametiwa
nguvuni na taasisi hiyo kwa mahojiano zaidi.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza yupo katika ziara kujitambulisha katika mkoa huo na
hii ikiwa ni Wilaya yake ya tatu mara baada yakutembelea wilaya za
Misungwi na Magu hapo awali.
Imetolewa na
Atley J. Kuni
AFISA HABARI NA MAHUSIANO –RS MWANZA. 18 Aprili, 2016
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment