Mwenyekiti
wa taifa wa Chama cha TLP na aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la
Vunjo, Agustino Mrema anatarajia kusafiri kuja jijini Dar es salaam kwa
lengo la kumpongeza Rais Magufuli na kumkumbusha ahadi aliyompa mwaka
jana ya kumpatia kazi Serikalini.
Akizungumza
kupitia kipindi cha Sun Rise kinachoruka kupitia Times fm, Mrema
amempongeza Rais kwa jitihada za ukusanyaji kodi na kupambana na Ufisadi
kwa nguvu.
“Tuweke
itikadi pembeni Rais wa sasa anaweka juhudi katika kukusanya kodi, na
mimi nilikuwa napiga nalo sana kelele hili swala, ila akipewa
ushirikiano baada ya miaka mitano tutasheherekea mafanikio yake.
“Wiki
ijayo natarajia kuja Dar, na nafikiri nitaonana na Rais kwanza
nimpongeze alafu nimsisitize anipe nafasi kuna sehemu nazijua
tuzisafishe, siwezi kusema mpaka nionane nae ndio nitamueleza”.
Mrema
pia alijivunia rekodi yake ya uongozi katika Serikali ya Tanzania, kama
kigezo kimoja wapo cha kumpatia ‘Chambirecho’ ya kupewa nafasi katika
Serikali ya Magufuli.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment