Meya wa jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita
Naibu
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, anatarajiwa kupatikana leo katika kikao
cha kwanza cha Baraza la Jiji kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa
Karimjee.
Uchaguzi
wa naibu meya unafanyika baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata
meya wa jiji hilo uliohitimishwa Machi 22, mwaka huu kufuatia kutawaliwa
na ‘figisufigisu’ kati ya CCM na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) zilizosababisha uaharishwe mara tatu.
Katika
kinya’nga’nyiro hicho, Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), Isaya
Mwita aliibuka kidedea kwa kupata kura 84 dhidi ya Diwani wa Kata ya
Mburahati (CCM), Yusuph Yenga aliyepata kura 67.
Meya
wa jiji hilo, Isaya Mwita jana alisema kuwa, maandalizi ya kikao hicho
kitakachokuwa na ajenda ya uchaguzi wa kumpata naibu meya yamekamilika.
Wagombea nafasi hiyo ni Kafana Mussa wa (CUF) na Mariam Lulida wa CCM.
Tofauti
na uchaguzi wa meya, uchaguzi wa leo hautarajiwi kuwa na mvutano mkubwa
baina ya Ukawa na CCM kwa kuwa haujumuishi madiwani wote wa jiji hilo,
isipokuwa kitakuwa na wajumbe 18.
Kati
ya wajumbe hao, kila manispaa itatoa wajumbe wanne wakiwamo mameya,
wakati wabunge watano wa majimbo wataruhusiwa kuingia kwenye baraza hilo
litakalokuwa chini ya uongozi wa meya huyo mpya.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment