April 12 2016, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
ametoa maagizo kwenye mambo matatu wakiwemo ombaomba wa mabarabarani,
majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipo kuwa na parking
na wamiliki wa bar kupiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.
Paul
Makonda ametoa siku sita mpaka April 18 ombaomba ndani ya Dar es salaam
kuondoka mabarabarani, wamiliki wa majengo walipe faini na kuweka
utaratibu wa magari yatapark wapi au kubomoa majengo yao, na kuhusu
wamiliki wa Bar Paul Makonda ameyazungumza haya……
>>>’wamiliki wa bar wanaowapigia watu kelele wafuate sheria walizopewa kama
ni mwisho saa sita kupiga muziki iwe hivyo na muziki huo upigwe kwenye
maeneo husika, mtu ambaye anapiga muziki nje ya utaratibu wa kibali
chake maana yake ajiandae kunyang’anywa leseni na kufutiwa kibali chake
na faini hiyo atailipa mwenyewe’:-Paul Makonda
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment